Chake Chake

Chake Chake
Chake Chake is located in Tanzania
Chake Chake
Chake Chake

Mahali pa mji wa Chake Chake katika Tanzania

Majiranukta: 5°14′24″S 39°46′12″E / 5.24000°S 39.77000°E / -5.24000; 39.77000
Nchi Tanzania
Mkoa Pemba Kusini
Wilaya Chake Chake
Ofisi ya Serikali katika Mji wa Chake Chake

Chake Chake ni mji mkubwa kwenye kisiwa cha Pemba ambacho ni sehemu ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni makao makuu ya wilaya ya Chake Chake katika mkoa wa Pemba Kusini (South Pemba).

Katika kata tatu za Chachani, Tibirinzi na Wara kuna takriban wakazi 15,000.

Mji umeenea kwenye kilima juu ya hori inayoingia ndani ya kisiwa. Bandari ya Chake Chake haina kina cha kutosha kwa meli hivyo hutumiwa na jahazi au dau ndogo tu.

Kitovu cha mji ni eneo la sokoni penye maduka, hospitali, boma la kale na hoteli ya SMZ. Kando la mji kuna uwanja mpya wa michezo na hospitali mpya.

Uwanja wa ndege wa Wawi uko kilomita saba kutoka mjini upande wa mashariki. Huo ni uwanja wa ndege wa pekee kisiwani ukihudumia ndege ndogo tu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne