Chasi (au Kialagwa au Algwaisa) ni mojawapo ya lugha za Kikushi zinazotumika nchini Tanzania. Inazungumzwa na Wasi: kabila hili sehemu zote wanazokaa wenyewe huongea lugha hii na ndiyo asili yao ya wazazi wao waliowakuta. Lugha hii si ya Kibantu, kwani huendana na Kifiomi, Kiiraqw na Kiburunge.
Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kialagwa imehesabiwa kuwa watu 30,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi Kialagwa iko katika kundi la Kikushi.