Jiji la Chicago | |||
| |||
Mahali pa mji wa Chicago katika Marekani |
|||
Majiranukta: 41°50′26″N 87°40′46″W / 41.84056°N 87.67944°W | |||
Nchi | Marekani | ||
---|---|---|---|
Jimbo | Illinois | ||
Wilaya | Cook | ||
Idadi ya wakazi | |||
- Wakazi kwa ujumla | 8,711,000 | ||
Tovuti: www.cityofchicago.org |
Chicago ni mji mkubwa wa jimbo la Illinois na pia mji mkubwa wa tatu nchini Marekani, bada tu ya New York na Los Angeles. Iko kando ya Ziwa Michigan. Idadi ya wakazi ni 2,900,000 (2000); pamoja na rundiko la mji ni watu milioni tisa.
Ni mji muhimu wa biashara na viwanda. Kwa kuwa meli za Atlantiki zinafika Chicago kupitia njia ya maji ya Saint Lawrence na pia ni chanzo cha reli muhimu huitwa mara nyingi "geti la magharibi" la Marekani. Kabla ya kujengwa kwa reli mfereji muhimu uliunganisha mji na mto Mississippi.
Chanzo cha Chicago kilikuwa kituo cha biashara kwenye mdomo wa mto Chicago. Mji uliundwa 12 Agosti 1833 ukawa manispaa 1837. Wakazi waliongezeka haraka. Walikuwa 30,000 mwaka 1850, 100,000 mwaka 1860 na hadi 1880 waliongezeka kuwa 500,000. Milioni ilifikwa 1890.
Kwa miaka mingi (kati ya 1974 hadi 1998) jengo la Sears Tower lilikuwa kubwa kuliko yote duniani likiwa na kimo cha mita 442.