Daa-mboo | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Daa-mboo (Priapulus caudatus)
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Ngeli 4: |
Daa-mboo (kutoka kwa Kiing. penis worm) ni wanyama wadogo wa bahari wa faila Priapulida wanaofanana na daa wa kawaida. Jina la kisayansi linatoka kwa Πριάπος – Priapos, mungu wa uzalishaji wa Wayunani, kwa sababu umbo wa daa hao ni kama mboo wa mtu. Huishi katika matope ya sakafu ya bahari mpaka kina cha m 90[1]. Spishi fulani zina uvumilivu wa ajabu kwa sulfidi ya hidrojeni na kwa uhaba wa oksijeni[2]. Wanaweza kuwa wengi sana katika baadhi ya maeneo. Katika Ghuba ya Alaska wapevu kama 85 wa Priapulus caudatus kwa mita ya mraba wamerekodiwa, huku idadi ya lava wake ikiweza kuwa hadi 58,000 kwa m2[3].
Wanyama hao wanaofanana na minyoo wana umbo la mcheduara na urefu wa sm 0.2-0.3[4] hadi 39[5]. Wana mdomo kwenye ncha ya mbele usio na silaha yoyote au minyiri. Mwili umegawanywa katika kiwiliwili kikuu na sehemu ya mkonga iliyovimba kidogo na kupambwa kwa vituta vinavyopita kutoka mbele hadi nyuma. Mwili una miviringo na mara nyingi huwa na duara za miiba ambazo zinaendelea kwenye koromeo inayoweza kujitokeza kidogo. Spishi fulani zinaweza pia kuwa na mkia au jozi ya viambatisho kwenye ncha ya nyuma. Mwili una kutikulo ya khitini inayobambuliwa mnyama akikua[6].
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)