Daktari (au dokta; wingi wake unaundwa kwa kutanguliza ma-) ni neno lenye asili ya Kilatini ("doctor") lililoingia Kiswahili kwa kupitia Kiingereza. Hutumiwa kwa maana mbili:
1) Mtaalamu aliyepata mafunzo maalum kwenye chuo kikuu cha kutibu maradhi ya wagonjwa. Mtu wenye ujuzi wa kutibu anaitwa pia mganga (wa), tabibu (ma). Daktari humtibu mgonjwa kwa kutumia sindano, kumtundikia dripu n.k. baada ya kumpima baadhi ya vitu kama:
2) Kwa kufuata tabia za lugha nyingine daktari hutumiwa pia kama jina la heshima kwa mtu aliyepata shahada ya uzamivu au "PhD" ambayo ni shahada ya juu kabisa.