Daniel Camille Victor Marie Labille (15 Oktoba 1932 – 31 Desemba 2022) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki nchini Ufaransa.
Alizaliwa nchini Ufaransa akapadrishwa mwaka 1956. Labille alihudumu kama askofu wa jimbojina la Fata na askofu msaidizi wa Dayosisi ya Soissons kutoka 1978 hadi 1984, kisha akawa askofu wa dayosisi hiyo kutoka 1984 hadi 1998.
Baadaye, alihudumu kama askofu wa Dayosisi ya Créteil kutoka 1998 hadi alipoastaafu mwaka 2007.[1]