Defao

Defao
Jina la kuzaliwa Matumona Defao Lulendo
Amezaliwa (1958-12-31)Desemba 31, 1958
Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Aina ya muziki Soukous, muziki wa dansi
Kazi yake mwimbaji/mtunzi wa nyimbo, mwanamuziki
Ala Sauti, gitaa
Miaka ya kazi 1976 - 2021
Ame/Wameshirikiana na Orchestre Suka Movema, Fogo Stars, Bozi Boziana, Grand Zaiko Wawa, Pepe Felix Manuaku

Francoise Lulendo Matumona (anajulikana kama General Defao; 31 Desemba 1958 - 27 Desemba 2021) alikuwa mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni miongoni mwa waimbaji wa Kikongo wenye majina makubwa.

Kazi zake za muziki hasa alizifanyia hukohuko kwao Kongo. Alianza kuimba mwaka 1976 kwenye makundi madogomadogo, huko mjini Kinshasa. Waliomvutia kuingia katika muziki kwa kipindi hicho ni Papa Wemba, Nyoka Longo, Gina Efonge Evoloko na waimbaji wanne wa kundi la Zaiko la miaka ya sabiini. Lakini yule hasa aliyemvutia akiimba ni Tabu Ley Rochereau. Tangu mwaka 1991, amenzisha bendi yake mwenyewe, The Big Stars, kwa lengo la kuwa nyota wa Afrika. Alifanya hili kwa kuwa nchini mwao ukishindwa kutimiza jambo fulani watu wanakucheka na huona wivu wengine wakifanikiwa - ndiyo-maana anafanya juhudi kubwa ili tu apate mafanikio.

Hayo yametokea kwa sababu asilimia kubwa wanamuziki wa Kongo hawana subira. Wanataka kila kitu harakaharaka. Sasa hivi katika umri wake miaka hamsini, Defao anachukulia mambo kadiri yanavyokuja na si kwa pupa tena. Anajua ya kwamba, kwake, kibao kitamgeukia. Defao alikufa mnamo Desemba 27, 2021 katika hospitali ya Laquintinie huko Douala, akiwa na umri wa miaka 62, kutokana na Covid-19.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne