Dhoruba

Dhoruba ya Vumbi, Texas (1935)
Dhoruba ikiambatana na radi

Dhoruba (kutoka neno la Kiarabu) ina maana ya hali ya hewa yenye ghasia, kwa kawaida huambatana na mvua kubwa na upepo.

Vimbunga vya bara la Amerika (kwa Kiingereza hurricane), vimbunga vya bara la Asia (kwa Kiingereza typhoon) na vimbunga vya bara la Afrika (kwa Kiingereza cyclone), mara nyingi, huitwa dhoruba pia, lakini vina majina maalumu kwa sababu vina nguvu sana.

Dhoruba inachunguzwa na wanasayansi wanaoitwa wapimaji wa hali ya hewa. Dhana ya utabiri wa ubaharia ilianza kwa wasiwasi wa kuokoa meli kutokana na dhoruba zisizotarajiwa katika Atlantiki ya Kaskazini.

Dhoruba inahusishwa na hali ya hewa yenye ghasia na inaweza kuwa na upepo mkali, ngurumo, radi na mvua kubwa kama vile ya barafu. Kwa hiyo, ujuzi wa hali ya hewa ni muhimu sana.

Kuna aina nyingi na majina ya dhoruba: dhoruba ya barafu, dhoruba ya theluji, dhoruba baharini, moto, n.k. Dhoruba ziitwazo dhoruba za ngurumo zinakua katika maeneo yenye joto na unyevunyevu, kama ya India. Joto la kupanda linazalisha upepo wenye nguvu ya uelekeo wa juu. Upepo huu hubeba matone ya maji juu, ambapo hufungia, na kuanguka tena. Katika harakati ya kuanguka, matone ya maji pamoja na kupanda juu kwa hewa kuunda mwanga na sauti.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dhoruba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne