Dini za jadi ni dini za mababu ambazo zinafuata miiko na maadili halisi ya taifa au kabila fulani.
Katika bara la Afrika dini hizo zinaegemea zaidi kwenye matambiko kwa mizimu ya ukoo ili isaidie jamaa zao.
Siku hizi idadi ya wafuasi wa dini hizo inazidi kupungua na kuziachia nafasi dini za kimataifa, hasa Ukristo na Uislamu.
Hata hivyo mabaki ya imani ya asili yanawaandama waliojiunga na dini hizo, hasa kwa namna inayotazamwa nazo kuwa ushirikina.