Disc jockey (kifupi "DJ") ni mtu anayeunganisha miziki kadhaa ikicheza, mara nyingi kwenye hadhira walio kwenye klabu au mtandao au kwenye matangazo. DJ huweza pia kutengeneza kandamseto zinazouzwa baadaye. Kwenye Hip hop "ma dj" hutengeneza midundo kwa kutumia piano, gitaa na "beats".