Domodomo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Domodomo wa Peters (Gnathonemus petersii)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 21:
|
Domodomo ni samaki wa maji baridi wa nusufamilia Mormyrinae katika familia Mormyridae na ngeli Actinopterygii (mapezi yenye mihimili) ambao wanatokea Afrika tu. Spishi nyingi zina pua ndefu na/au mdomo wa chini mrefu. Kwa hivyo inaonekana kama zina aina ya mwiro na kwa sababu ya hiyo jina lao kwa Kiingereza ni “elephantfish”, “tapirfish” au “trunkfish”. “Mwiro” huo hutumika kwa kusikia invertebrata katika matope. Spishi zenye pua au mwiro mfupi kiasi huitwa mputa kwa kawaida. Majina mengine ni linjolo, mbete, mbelewele, mpuni, nchemba, ndaka na ntachi.
Nusufamilia hii ina zote ila moja za jenasi za Mormyridae. Ni nusufamilia kubwa kabisa katika oda Osteoglossiformes ikiwa na takriban spishi 170. Spishi hizi zina uwiano mkubwa kati ya masi ya ubongo na ile ya mwili kwa sababu ubongonyuma umevimba na hutumika katika udakaji wao wa umeme. Zaidi ya hao zinajulikana kwa kushikilia rekodi ya zoolojia ya takriban 60% iliyo ni asilimia ya nishati unayotumia ubongo wao ikilinganishwa na mwili mzima. Kabla ya ugunduzi huu, ilikuwa ubongo wa kibinadamu ambao ulifikiriwa kushikilia rekodi hii lakini kwa ukweli hutumia 20% tu.