Dr. Dre | |
---|---|
![]() Dr. Dre mnamo 2011
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Andre Romelle Young |
Amezaliwa | 18 Februari 1965 |
Asili yake | Los Angeles, California, Marekani |
Aina ya muziki | Hip hop, West Coast hip hop, Electronic rap, Gangsta funk, Gangsta rap |
Kazi yake | Rapa, mtayarishaji wa rekodi |
Ala | Sauti, synthesizer, Kinanda, fonografia, mashine ya ngoma |
Miaka ya kazi | 1984–hadi leo |
Studio | Epic, Ruthless, Priority, Death Row, Aftermath, Interscope |
Ame/Wameshirikiana na | Eazy E, Ice Cube, The D.O.C, Snoop Dogg, N.W.A, 2Pac, Eminem, 50 Cent, The Game, Shade Sheist, Busta Rhymes, Xzibit, Royce Da 5'9", Jay-Z, Nas, Blackstreet, Stat Quo, Bishop Lamont, MC Ren, Obie Trice |
Tovuti | Dre2001.com |
Andre Romelle Young (alizaliwa tar. 18 Februari 1965) ni mtayarishaji wa rekodi, rapa, na mmiliki wa studio ya rekodi za muziki kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Dr. Dre. Dre ni mwanzilishi na mmiliki wa sasa Aftermath Entertainment na mmiliki mshiriki-msanii wa zamani wa studio ya Death Row Records, na pia kutayarisha albamu kadhaa kwa ajili yake na wasanii wengine kadhaa wa rekodi hiyo kama vile Snoop Dogg na Eminem.
Akiwa kama mtayarishaji, amejipatia sifa sana kwa kuukuza muziki wa West Coast G-funk, staili ya muziki wa rap unaotengenezwa na synthesizer-yenye ya taratibu, na mdundo wa nguvu.
Dr. Dre alianza shughuli za muiki akiwa kama mmoja kati ya wanamchama wa kundi la muziki la World Class Wreckin' Cru na kisha baadaye akaanzisha kundi lenye athira kubwa ya gangsta rap la N.W.A, ambayo ilivuma sana kwa mashairi yake mazito yenye kutaja maisha ya kiharifu na mtaani kwa ujumla.[1] Mnamo mwaka wa 1992, alitoa albamu kama msanii wa kujitegemea. Na albamu ilikwenda kwa jina la The Chronic, ilitolewa ikiwa chini ya Death Row Records, na kumpelekea kuwa mmoja katia ya wasanii waliouza rekodi bora za muziki wa Marekani kwa mwaka wa 1993[2] na kushinda Tuzo ya Grammy kwa ajili ya single ya "Let Me Ride".
Mnamo mwaka wa 1996, aliondoka Death Row na kwenda kuanzisha studio yake mwenyewe ya Aftermath Entertainment, na kutoa albamu ya mchanganyiko ya Dr. Dre Presents the Aftermath, kunako 1996, na ksiha baadaye akatoa albamu yake nyingine iliyokwendwa kwa jina la 2001, kunako 1999, ambayo ili mfanya ashinde Tuzo ya Grammy akiwa kama mtayarisha bora.
Kunako miaka ya 2000, aliekeza shughuli zake za utayarishaji wa muziki kwa wasanii wengine, wakati muda huo akawa anashiriki katika kutia sauti kwenye baadhi ya nyimbo za wasanii wengine.
Rolling Stone wamemwita ni mmoja kati ya wasanii waliolipwa pesa nyingi sana kwa mwaka wa 2001[3] na 2004.[4] Dr. Dre also had acting roles in the 2001 films The Wash and Training Day.[5]
{{cite web}}
: Unknown parameter |=
ignored (help); Unknown parameter |coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help)
{{cite web}}
: Unknown parameter |=
ignored (help) Ilihifadhiwa 2 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine.