26°10′38″S 28°13′19″E / 26.17722°S 28.22194°E
East Rand ni upande wa mashariki wa Witwatersrand. Imeunganika na Johannesburg, mkoa wa Gauteng, nchini Afrika Kusini. Eneo hilo lilianza kukaliwa na Wazungu mwaka 1886 kutokana na upatikanaji wa migodi ya dhahabu uliosababishwa kuundwa kwa Johannesburg.
Eneo hilo linaanzia Germiston hadi Springs na Nigel, likijumuisha miji ya Boksburg, Benoni, Brakpan, Kempton Park, Edenvale na Bedfordview.