Edburga wa Winchester (jina asili: Eadburh; alifariki 15 Juni 960) alikuwa binti wa mfalme wa Uingereza Edward Mzee na wa mke wake wa tatu, Eadgifu wa Kent.
Maisha yake yaliandikwa kwanza na Osbert de Clare, aliyepata kuwa priori wa Westminster mwaka 1136.[1]
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.[2]
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana tarehe ya kifo chake.