Ekari (kwa Kiingereza: acre) ni kipimo cha eneo cha Kiingereza kinachotumiwa pia Marekani na bado kuwa kawaida katika nchi zilizokuwa koloni za Uingereza. Kwa kawaida hutumiwa kutaja maeneo ya ardhi, mashamba na viwanda.
Asili ya istilahi ni neno la Kiingereza linalomaanisha shamba linaloweza kulimwa kwa siku ukitumia plau na maksai.