Eladi wa Auxerre (kwa Kifaransa: Hellade; alifariki Auxerre, leo nchini Ufaransa, 388) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 365 hadi kifo chake[1][2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 8 Mei[3][4].