Elimu ya visasili

Prometheus: mchoro huu wa mwaka 1868 wa Gustave Moreau unamuonyesha amefungwa na kuteseka kwa kosa la kuwapa binadamu moto kama kiumbe chake, inavyosimuliwa na visasili na fasihi ya Kigiriki.

Elimu ya visasili (au mithiolojia, Kiing. mythology, kutoka neno la Kigiriki μυθολογία, mithologia, linaloundwa na μῦθος, mithos, "kisasili" na λογία, logia, "elimu") inahusu utafiti juu ya visasili vya makabila mbalimbali ili kuelewa utamaduni wao.

Jinsi visasili vilivyoanza haijulikani vizuri, lakini vimekuwa vimechunguzwa tangu kale, kwa mfano huko China na Ugiriki wa Kale.

Juhudi kubwa zaidi za kuzilinganisha zilifanywa kuanzia karne ya 19 kwa mitazamo tofauti, chanya au hasi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne