| |
Tarehe ya kuzaliwa | 21 Aprili 1926 |
Mahali pa kuzaliwa | Mayfair, Uingereza Ufalme wa Muungano |
Tarehe ya kifo | 8 Septemba 2022 (umri 96) |
Elizabeth II alikuwa malkia wa Ufalme wa Muungano wa Britania (Uingereza na Welisi na Uskoti) na Ireland Kaskazini tangu mwaka 1952 hadi kufariki dunia tarehe 8 Septemba 2022. Alikuwa malkia kwa miaka 70 na siku 214. Katika historia yote ya dunia wako watawala wachache waliodumu madarakani muda mrefu kuliko yeye[1][2]. Soma zaidi wasifu wake hapa Anafuatwa na mwana wake wa kwanza, Charles III wa Uingereza.
Alizaliwa kwa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor mjini London tarehe 21 Aprili 1926 kama mtoto wa kwanza wa mfalme George VI wa Uingereza na Elizabeth Bowes-Lyon.
Alitangazwa kuwa malkia tarehe 6 Februari 1952 mara moja baada ya kifo cha baba yake George VI. Wakati ule alikuwa akitembelea Kenya iliyokuwa bado koloni la Uingereza akatembelea milima ya Aberdare.
Alipokea taji katika ibada rasmi tarehe 2 Juni 1953 kwenye kanisa la Westminster Abbey.
Kama mkuu wa Jumuiya ya Madola alikuwa pia mkuu wa dola wa nchi zifuatazo ndani ya jumuiya hii[3]:
Katika nchi zote aliposhika cheo hakuwa na mamlaka ya kiserikali ila alitawala kama mfalme wa kikatiba katika muundo wa serikali ya kibunge.