Engrasya (Braga, Ureno, karne ya 3 - Zaragoza, Hispania, 304 hivi) alikuwa bikira aliyestahimili mateso na kifodini katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano dhidi ya Wakristo [1]. Siku hizi wengine wanamtaja kaisari Valerian (254-260)[2]
Heshima ya watu kwake kama mtakatifu ni ya zamani sana. Mshairi Prudentius (348-410), mwenyeji wa mji huo, alitunga utenzi juu yake na ya wafiadini wenzake[3].
Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 16 Aprili[4].