Eoni wa Arles (Chalon-sur-Saône, karne ya 5 BK - Arles, 17 Agosti 502) alikuwa askofu wa mji huo (leo nchini Ufaransa) kuanzia mwaka 485 hadi kifo chake .
Alilinda Kanisa lake dhidi ya uzushi wa Pelaji akapendekeza kwa waumini wake wamfanye mwandamizi wake Sesari[1], ambaye mwenyewe alikuwa amempa upadirisho [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.