Euro ni sarafu ya pamoja katika baadhi ya nchi za Ulaya. Wakazi wake 350,000,000 (2023) wanatumia kwa kawaida pesa hiyo. Watu wengine 210,000,000 wanatumia pesa zilizoungwa na euro, hasa barani Afrika.
Tangu mwaka 2002 nchi 13 za EU zilifuta sarafu ya kitaifa ili kutumia Euro tu. Siku hizi ni 20.
Euro moja imegawanyika katika senti 100.
Kuna benknoti za € 5 (kijivu), € 10 (nyekundu), € 20 (buluu), € 50 (machungwa), € 100 (kijani), € 200 (njano), € 500 (nyekundu).
Kuna sarafu za metali 8 za € 0,01, € 0,02, € 0,05, € 0,10, € 0,20, € 0,50, € 1, € 2.
Pesa ya karatasi inatolewa na benki kuu ya Ulaya na ni sawa kote.
Sarafu zinatolewa na nchi wanachama na zinatofautiana upande mmoja, lakini sarafu zote hutumika kote.