Eusebia wa Hamay (637 - 660) alikuwa bikira ambaye, baada ya kufiwa baba yake alijiunga na monasteri ya Hamay pamoja na mama yake, Riktrude, akaja kuwa abesi wake akiwa na umri wa miaka kumi na miwili tu kufuatana na kifo cha bibi yake Getrude (649)[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu kama hao na ndugu zao wengi.