Eutropia wa Aleksandria (alifia dini 250 hivi) alikuwa mwanamke wa mji huo (nchini Misri) ambaye aliuawa kikatili sana wakati wa dhuluma ya kaisari Decius kwa kuwa alikataa kumkana Kristo. Inasemekana hatimaye alikatwa kichwa[1][2].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Oktoba[3][4].
Inawezekana kuwa ni yuleyule anayeheshimiwa siku hiyohiyo kwa jina la Eutropia wa Afrika Kaskazini[5].