Eva

Eva akiinama kula tunda, alivyochongwa na Gislebertus upande wa nje wa kanisa kuu la Autun, Ufaransa.

Eva ni jina la mwanamke wa kwanza kadiri ya Biblia. Maana yake inafikiriwa kuhusiana na uhai: mama wa walio hai.

Kanisa Katoliki linamheshimu kama mtakatifu tarehe 24 Desemba[1].

Umaarufu wake umeongezeka tena hivi karibuni, baada ya upimaji wa DNA ya mviringo kuthibitisha kwamba binadamu wote wanatokana na mama mmoja.

  1. https://catholicsaints.info/eve-the-matriarch/

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne