Fabaceae | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Ua la Centrosema pubescens, mmea kwenye familia ya Fabaceae
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusufamilia 6:
|
Fabaceae au Leguminosae, inayojulikana kama familia ya mimea ya jamii ya mkunde na mimea aina ya mharagwe, ni familia kubwa ya mimea yenye maua iliyo na umuhimu kiuchumi na kibiolojia. Familia hii inajumuisha miti, vichaka na mimea ya muda na ya msimu, na inatambuliwa kwa urahisi kwa kupitia matunda (kunde) na majani yake. Mimea mingi ya jamii ya mkunde ina maua na matunda ya kipekee.
Familia hii imesambaa maeneo mengi duniani na ni familia ya tatu kwa ukubwa kwa mimea ya nchi kavu kwa kuzingatia idadi ya spishi, ikipitwa na familia ya Okidi na Asteraceae pekee. Inajumuisha takribani jenasi 751 zenye spishi zipatazo 19,000. [1] [2]
Jenasi tano kubwa zaidi za familia hii ni Astragalus (zaidi ya spishi 3,000), Acacia (spishi zaidi ya 900), Indigofera (karibu spishi 700), Crotalaria (spishi karibu 700), na Mimosa (karibu spishi 400). Jenasi hizi kwa pamoja zinabeba walau robo ya spishi zote za mimea ya jamii ya mkunde. Spishi 19,000 za jamii ya mkunde zinazojulikana hadi sasa kwa pamoja zinatengeneza karibu 7% ya spishi zote za mimea yenye maua. [3] Mimea ya familia hii ndiyo inayopatikana kwa wingi zaidi katika misitu ya mvua ya kitropiki na misitu kavu ya Amerika na Afrika. [4]
Tafiti za hivi karibuni zilizotumia njia za kimolekula na maumbile zinaonyesha kwamba familia ya Fabaceae ni kundi la kijenetiki kutoka kwa mhenga mmoja. [5] Swala hili linapata mkazo kutokana na uhusiano kati ya makundi ya mimea ndani ya familia hii, uhusiano wa familia hii mimea inayokaribiana nayo pamoja na tafiti za jenetika zinazotumia Asidi Kiinideoksiribo.[6][7][8]. Tafiti hizi zimeonyesha kwamba mimea ya familia ya Fabaceae ni kundi lenye jadi moja linalohusiana kwa ukaribu na familia za Polygalaceae, Surianaceae na Quillajaceae ambazo kwa pamoja zipo chini ya oda ya Fabales.[9]
Baadhi ya mimea ya familia ya Leguminosae imekua chanzo kikuu cha chakula cha binadamu kwa milenia nyingi pamoja na nafaka, baadhi ya matunda na vyakula vya mizizi vya kitropiki. Matumizi ya vyakula hivi yanahusiana kwa ukaribu na mageuko ya binadamu.[10] Familia hii inajumuisha mimea mingi yenye umuhimu kwanye kilimo na chakula, ikiwemo Glycine max (maharagwe ya soya), Phaseolus (maharagwe), Pisum sativum (njegere), Cicer arietinum (njegere kubwa), Medicago sativa (luseni), Arachis hypogaea (karanga), Ceratonia siliqua (karuba), na Glycyrrhiza glabra. Spishi nyingine za familia hii zinatambulika kama magugu sehemu mbali mbali duniani zikiwemo: Cytisus scoparius, Robinia pseudoacacia, Ulex europaeus, Pueraria montana, na baadhi ya spishi za jenasi Lupinus.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: DOI inactive as of 2021 (link) CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite journal}}
: Unknown parameter |dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: Unknown parameter |dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)