Fani

Kwa matumizi tofauti ya neno hili angalia makala Fani (fasihi)

Fani (kutoka ar. فنع "bora") ni uwanja maalumu wa elimu, maarifa au kazi. Kutaja kazi fulani kuwa "fani" kunahitaji kiwango fulani wa ubora au taaluma.

Mifano ya fani katika ufundi ni pamoja na useremala, ujenzi, uhunzi, upishi au uchoraji.

Mifano ya fani katika sayansi au elimu ya juu ni pamoja na

  • sayansi asilia kama vile fizikia, kemia, astronomia, biolojia, tiba
  • sayansi jamii kama vile historia, ualimu, falsafa, isimu, fasihi, sosholojia

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne