Farakano la Kanisa la Magharibi lilitokea ndani ya Kanisa Katoliki katika miaka 1378-1418.
Makardinali wenye jukumu la kumchagua Papa walichagua wawili, mmoja baada ya mwingine, na hivyo kusababisha isieleweke yupi ana haki ya kuongoza.
Siasa ilijiingiza na kudumisha fujo kubwa, ingawa si kuhusu mafundisho ya imani, mpaka Mtaguso wa Konstanz (1414–1418) ulipotoa suluhisho.
Hata hivyo ilibaki athari mbaya juu ya mamlaka ya Mapapa waliofuata.