Farao

Farao.

Farao (kwa Kimisri jumba. Katika lugha ya Kiswahili linatumika pia jina Firauni) lilikuwa jina la heshima ambalo kila mfalme wa Misri ya kale alipewa. Jina hilo lilitumika hadi Warumi walipoiteka Misri mwaka 30 KK. Kabla ya hapo, wafalme wa kale wa Misri walikuwa na majina matatu: Horus, Nesu Bety na Nebty.

Maarufu zaidi ni Ramses II aliyekuwa farao wa masimulizi ya Biblia na Kurani kuhusu Musa, pamoja na Tutankhamun ambaye ni farao pekee ambaye kaburi lake limehifadhiwa hadi leo bila kuporwa na majambazi.

Farao wa mwisho alikuwa malkia Kleopatra.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne