Fasihi andishi ni sanaa itumiayo maandishi kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.
Fasihi andishi hugawanyika katika matawi mawili: nathari na ushairi.
Pia fasihi andishi ina tanzu nyingi mbalimbali, hasa hadithi fupi, riwaya, tamthiliya, insha, shairi n.k.
Kulingana na mada ya kazi ya kifasihi, inawezekana kutofautisha bunilizi na kazi zinazowakilisha ukweli.