Felisi na Fortunati

Kifodini cha Wat. Felisi na Fortunati,
mchoro wa Gaspare Diziani, 1740 hivi.

Felisi na Fortunati (walifariki Aquileia, Friuli, leo nchini Italia, mwanzoni mwa karne ya 4) walikuwa ndugu Wakristo kutoka Vicenza ambao waliuawa kwa kukatwa kichwa kutokana na imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao ni tarehe 14 Mei[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91154
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne