Filemoni

Mchoro mdogo wa kifodini cha Filemoni, Afia na Onesimo.

Filemoni pamoja na mke wake Afia alikuwa kati ya Wakristo wa kwanza wa mkoa wa Frigia (karne ya 1).

Ni maarufu hasa kwa kupokea barua ya Mtume Paulo kuhusu mtumwa wake Onesimo ambaye alikuwa amemtoroka na labda kumuibia. Kumbe alipokutana na Paulo aliongokea Ukristo. Hapo alirudishwa kwa Filemoni akileta hiyo barua ambayo baadaye iliingia katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo kama Waraka kwa Filemoni.

Inaonekana humo kwamba Filemoni alikuwa tajiri wa mji wa Kolosai ambaye Wakristo wa huko walikuwa wanakusanyika nyumbani mwake kwa ajili ya ibada.[1][2][3] Paulo alifurahia upendo wake kwa Kristo [4].

Inasemekana aliuawa kwa ajili ya imani pamoja na mke wake na wengineo.

Kwa vyovyote anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Novemba[5].

  1. Const. Apost., VI, 46
  2. Filemoni 1:1-2
  3.  "Philemon" . Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  4. https://www.santiebeati.it/dettaglio/90445
  5. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne