Foilano (pia: Foillan, Faélán, Faolán, Foélán, Feuillen; Connacht, Ireland, 600 hivi - Msitu wa Soignes, leo nchini Ubelgiji, 31 Oktoba 655) alikuwa mmonaki padri wa Ukristo wa Kiselti aliyemfuata kaka yake[1] Fursei kufanya kazi kubwa kueneza imani na umonaki kotekote katika visiwa vya Britania, hasa kati ya Waanglia[2][3].
Baadaye alihamia Ufaransa alipoendelea kuinjilisha pamoja na kuanzisha monasteri ya kiume huko Fosses na ya kike huko Nivelles. Aliuawa na majambazi wakati wa kusafiri kutoka moja hadi nyingine[4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Oktoba[5].