Fransisko Serrano, O.P. (Hueneja, 4 Desemba 1695 – Fuzhou, 25 Oktoba 1748) alikuwa askofu mteule kutoka Hispania aliyefanya umisionari barani Asia akauawa nchini China kwa ajili ya imani yake ya Kikristo pamoja na mapadri Wadominiko wenzake Yohakim Royo, Yohane Alcober na Fransisko Diaz.[1][2]
Alitangazwa kuwa mtakatifu pamoja na wengine 119 waliofuata kifodini chake na Papa Yohane Paulo II tarehe 1 Oktoba 2000.[3]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Oktoba, lakini pamoja na wenzake ni tarehe 9 Julai[4].
{{cite web}}
: Unknown parameter |deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: unrecognized language (link)