Fransisko Diaz

Wafiadini Wakatoliki wa China.

Fransisko Diaz, O.P. (Ecija, 2 Oktoba 1713Fuzhou, 28 Oktoba 1748) alikuwa padri kutoka Hispania aliyefanya umisionari barani Asia akauawa nchini China kwa ajili ya imani yake ya Kikristo pamoja na mapadri Wadominiko wenzake Fransisko Serrano, Yohakim Royo na Yohane Alcober.[1][2]

Alitangazwa kuwa mtakatifu pamoja na wengine 119 waliofuata kifodini chake na Papa Yohane Paulo II tarehe 1 Oktoba 2000.[3]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, lakini pamoja na wenzake ni tarehe 9 Julai.

  1. "Saint Francis Ferdinand de Capillas". Patron Saints Index. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-06. Iliwekwa mnamo 2008-04-24.
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/92172
  3. "Den hellige Frans Fernández de Capillas (1607-1648)" (kwa Norwegian). katolsk.no. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-09. Iliwekwa mnamo 2009-04-24. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: unrecognized language (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne