Franz Liszt (22 Oktoba 1811 – 31 Julai 1886) alikuwa mtunzi wa Opera na mpigakinanda mashuhuri kutoka nchini Hungaria.
Amefahamika sana kwa ujuzi wake wa upigaji kinanda kwa haraka zaidi na kuwa na maarifa ya juu katika fani hiyo.
Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.