Frodobati (kwa Kifaransa: Frobert de Troyes; alifariki 673) alikuwa mwanzilishi[1] na abati wa kwanza wa monasteri ya Moutier-la-Celle huko Troyes katika Ufaransa wa leo[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Januari[3].