Gabrieli Taurin Dufresse, M.E.P. (Ville-de-Lezoux, Ufaransa, 8 Desemba 1750 - Chengdu, Sichuan, 14 Septemba 1815) alikuwa askofu mmisionari wa Kanisa Katoliki nchini China aliyefia Ukristo kwa kukatwa kichwa baada ya miaka 40 ya utume wenye bidii [1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao ya pamoja huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake tarehe ya kifodini chake[2].