Galus I wa Clermont (Clermont-Ferrand, leo nchini Ufaransa, 489 hivi - Clermont-Ferrand, 553 hivi) alikuwa askofu wa 16 wa mji huo kuanzia mwaka 527 hadi kifo chake[1].
Mtoto wa makabaila, alikataa ndoa akawa mmonaki mnyenyekevu na mpole. Kwanza alifanywa padri, halafu askofu, akaongoza kwa ufanisi mkubwa[2], kama ilivyoandikwa na Gregori wa Tours, aliyekuwa mwanafunzi wake na mwana wa ndugu yake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.