Giotto di Bondone (Florence, 1266/7 – 8 Januari 1337) ni kati ya wachoraji bora kutoka Italia, pamoja na kuwa mhandisi.
Anahesabiwa kati ya wasanii walioandaa Renaissance, kwa kuachana na mitindo ya Bizanti na kuchora watu walivyo kweli.[1]
Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.