Giza (Misri)





Giza

Bendera

Nembo
Giza is located in Misri
Giza
Giza

Mahali pa mji wa Giza katika Misri

Majiranukta: 30°01′0″N 31°13′0″E / 30.01667°N 31.21667°E / 30.01667; 31.21667
Nchi Misri
Mkoa Giza
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 2,443,490

Giza (pia: Gizeh, kutoka Kar.: الجيزة al-gīza) ni mji wa kaskazini ya Misri unaopakana na mji mkuu Kairo. Kuna wakazi 2,443,490 (2005).

Mji wa Giza waonekana kama mtaa wa Kairo tu lakini ni mji wa pekee. Zamani ilitengwa na mji mkuu kwa uwazi wa mashamba lakini siku hizi miji yote miwili imekua hadi kugusana kabisa.

Giza yajulikana hasa kama mahali pa piramidi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne