Gregori wa Langres

Gregori wa Langres (446 hivi – 539) alikuwa mtawala wa Autun, huko Ufaransa.

Baada ya kufiwa mke wake, akawa askofu wa Langres tangu mwaka 506 hadi kifo chake.

Gregori wa Tours alikuwa kitukuu wake.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni 4 Januari[1].

  1. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne