Haki za wanawake ni haki za binadamu zinazowalenga zaidi wanawake (na wasichana) duniani kote.
Vuguvugu la haki za wanawake lilianza karne ya 19. Haki hizo zinaungwa mkono na sheria, mila na desturi za jamii mbalimbali, ambapo katika nchi nyingine, haki hizo hazizingatiwi na hivyo hukandamizwa. Haki za wanawake zinatofautiana kutoka jamii moja kwenda nyingine kuendana na historia, utamaduni na desturi zilizozoeleka.[1]
Masuala ambayo kwa kawaida huhusishwa na dhana ya haki za wanawake ni pamoja na uhuru wa kujitawala, kutokuwa na unyanyasaji wa kijinsia, kupiga kura, kushika nafasi za uongozi, umiliki wa mali na kuingia mikataba ya kisheria.[2]