Hemikodata

Hemikodata
Mnyoo-mkonga (Glossobalanus sp.)
Mnyoo-mkonga (Glossobalanus sp.)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila ya juu: Deuterostomia
Faila: Hemichordata
Bateson, 1885
Ngazi za chini

Ngeli 3:

Hemikodata ni faila ya wanyama wa bahari katika faila ya juu Deuterostomia. Wanachukuliwa kama kikundi cha dada cha wanyama ngozi-miiba. Wanatokea kwa mara ya kwanza katika Cambrian ya Chini au ya Kati na wana ngeli kuu mbili: Enteropneusta (minyoo-mkonga) na Pterobranchia. Ngeli ya tatu, Planctosphaeroidea, inajulikana tu kutoka kwa lava wa spishi moja, Planctosphaera pelagica. Ngeli Graptolithina, iliyokwisha sasa, inahusiana sana na Pterobranchia.

Hemikodata ni kati ya jamaa wa karibu zaidi wa kijeni wa Kodata kati ya invertebrata. Kwa hivyo minyoo hao wa bahari ni ya kuvutia sana kwa utafiti wa asili ya maendeleo ya kodata.

Minyoo-mkonga huishi peke yao katika vishimo kwenye sakafu ya bahari (mirija ya kwanza ya kabla ya historia iliyotolewa) na hujilisha kwa mashapo. Lakini spishi kadhaa hutumia nyufa katika koromeo ili kuchuja chembe za chakula kutoka maji. Spishi za familia Torquaratoridae huishi huru na kujilisha kwa maada ogania kwenye sakafu. Pterobranchia huchuja chakula na minyiri yao. Huishi katika makoloni, muundo wa kolajeni kwa umbo la mrija unaoitwa coenecium.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne