Bonde la Honde linaanzia kutoka mpaka wa mashariki ya Zimbabwe hadi Msumbiji. Bonde hilo ni sehemu ya miinuko ya mashariki. Bonde hili lipo takriban kilomita 130 kutoka Mutare na kilomita 110 kutoka Nyaga. Milima ya Nyanga na mbuga za Nyanga kwa pamoja zinaunda mpaka wa magharibi wa bonde.