Huduma ya kwanza

Msalaba kati ya rangi ya kijani kibichi ni alama ya huduma ya kwanza kwa mfano kwenye kisanduku cha huduma ya kwanza chenye plasta na bendeji inayowekwa katika magari kwa nafasi za ajali.

Huduma ya kwanza inamaanisha huduma au msaada unatolewa kwa mtu anayekabiliwa na ugonjwa au madhara ya ghafla wakati daktari hayupo karibu na kabla hajapelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

Kwa mfano huduma ya kwanza inatolewa wakati mtu anapopatikana baada ya ajali amejeruhiwa kwa shabaha ya kutunza uhai wake hadi mganga atakapopatikana au mjeruhiwa atakapoweza kufikishwa hospitalini.

Shabaha nyingine ni kuzuia kuongezeka kwa madhara kwa mfano kwa kumwondoa sehemu yenye hatari kama moto, hatari ya mlipuko au mahali penye hatari kwake binafsi.

Huduma ya kwanza inaweza pia kutaja misaada midogo kama kumpatia mtu plasta ya kufunika kidonda kisicho kikubwa.

Katika nchi nyingi mtu yeyote anayefanya mtihani wa liseni ya kuendeshea gari anahitaji kuonyesha ya kwamba alihudhuria masomo kadhaa alipopata elimu ya msingi kuhusu huduma ya kwanza.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne