“I Wanna Be the Only One” | |||||
---|---|---|---|---|---|
![]() | |||||
Single ya Eternal wakishirikiana na BeBe Winans kutoka katika albamu ya Before the Rain | |||||
Imetolewa | 19 Mei 1997 | ||||
Imerekodiwa | 1996 | ||||
Aina | R&B, Muziki wa injili | ||||
Urefu | 4:18 (toleo la albamu) 3:36 (haririo la redio) | ||||
Studio | EMI | ||||
Mtunzi | BeBe Winans na James "Rhett" Lawrence | ||||
Mtayarishaji | Nigel Lowis | ||||
Mwenendo wa single za Eternal wakishirikiana na BeBe Winans | |||||
|
"I Wanna Be the Only One" ni jina la wimbo wa kundi la wasichana la muziki wa R&B kutoka nchini Uingereza Eternal. Huu ulikuwa wimbo wao wa tatu kutolewa kama single kutoka katika albamu yao ya Before the Rain. Mnamo mwezi Mei 1997, kundi limeunga nguvu na mwimbaji wa Kimarekani BeBe Winans. Wimbo ulifikia chati za juu sana kwenye UK Singles Chart. Kundi hilihili awali lilitamba nafasi ya kwanza #1 huko nchini Japan na vibao vyao kama vile "Stay", "Power Of A Woman", "Who Are You" na "Finally". Vilevile inakuwa mara ya pili kwa Winans kushirikiana na kundi kwa kufuatia mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1994 katika kibao chao cha "Crazy" kutoka katika albamu yao ya kwanza walioshinda maplatinamu kedekede Always & Forever.) ambamo alitayarisha na kutunga.
"I Wanna Be the Only One" umekuwa wimbo maarufu wa Eternal hadi leo hii: huu ulikuwa wimbo wa tatu kuchezwa sana katika redio huko nchini Uingereza na wimbo uliochezwa sana katika redio za Ulaya kutoka kwa wasanii wa Kiingereza kwa mwaka wa 1997. Wimbo umepelekea Eternal kupata Tuzo ya MOBO na Tuzo ya Capital FM ikiwa kama single bora. Vilevile ulipata kuchaguliwa kama Single Bora katika chati za BRIT Awards; ijapokuwa tuzo ilienda kwa wimbo wa "Never Ever" wa All Saints, ripoti zisizo rasmi zinasema mpambano ulikuwa mkali kiasi almanusura ushindi aidha uende kwa Eternal au Spice Girls. Na kwa mwezi Mei 2017, wimbo umeuza nakala 603,000 nchini Uingereza.[1]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)