Mt. Ida katika dirisha la kioo cha rangi .
Ida wa Herzfeld (770 hivi – 4 Septemba 825 ), wa ukoo wa kaisari Karolo Mkuu [ 1] , alilelewa ikulu kabla hajaolewa na Ekbert, mtawala wa Saksonia nchini Ujerumani .
Alimzalia watoto watano na kumhudumia katika ugonjwa wake mrefu[ 2] .
Baada ya kufiwa naye, alijitosa kuhudumia fukara kwa upendo na kusali kwa bidii [ 3] .
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu [ 4] .
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake [ 5] .
↑ Bring-Gould, Sabine. "S. Ida, W.", The Lives of the Saints , J. Hodges, 1882, p.50
↑ Butler, Alban. “Saint Ida, Widow”, Lives of the Fathers, Martyrs, and Principal Saints , 1866
↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/91888
↑ Clemens Hillmann. Die Kirche und Grabstätte der heiligen Ida von Herzfeld . Herausgegeben von der katholischen Pfarrgemeinde St. Ida Herzfeld, dcv druck Werl, 2. erweiterte und aktualisierte Aufl. 2003.
↑ Martyrologium Romanum