Ignas wa Antiokia (kwa Kigiriki Ἰγνάτιος, Ignatios; alijulikana pia kwa jina la Θεοφόρος, Theophoros, yaani "Mleta Mungu"; 35/50 B.K. - 98/117[1]).
Ni kati ya Mababu wa Kanisa wa kwanza, akiwa mwanafunzi wa Mtume Yohane na askofu wa tatu wa Antiokia, leo nchini Uturuki.
Chini ya kaisari Traiano, alihukumiwa kuliwa na wanyamapori, na kwa ajili hiyo alifikishwa Roma alipofia dini yake: safarini, huku akionja ukatili wa walinzi wake, alioufananisha na ule wa chui, aliandika barua kwa makanisa mbalimbali na kwa Polikarp Mtakatifu , alimohimiza ndugu zake katika imani kumtumikia Mungu katika ushirika na maaskofu na wasimzuie kuchinjwa sadaka kwa Kristo[2].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki[3][4], Waanglikana na Waorthodoksi wa Mashariki kwenye 17 Oktoba, lakini na Waorthodoksi tarehe 20 Desemba.