Ijumaa Kuu ni siku ya Ijumaa kabla ya Pasaka ambapo Wakristo wengi duniani wanaadhimisha kifo cha Yesu Kristo msalabani.
Kufuatana na taarifa za Injili nne katika Biblia ya Kikristo, Yesu alisulubiwa siku kabla ya Sabato (au Jumamosi), yaani Ijumaa. Mahali pa kumsulubisha palikuwa kilima cha Golgotha kilichokuwepo wakati ule nje ya kuta za mji wa Yerusalemu.