Ikonografia (kutoka Kigiriki εἰκών, eikon, "picha" na γράφειν, grafein, "kuandika" kupitia Kiingereza "iconography") ni tawi la historia ya sanaa ambalo linachunguza asili na maana ya picha kama sanaa[1][2][3].
Utaalamu huo unahitajika hasa katika kufafanua picha takatifu za Ukristo wa Mashariki, kwa kuwa hizo hazilengi kuiga sura halisi zinavyoonekana na macho, bali kudokeza mafumbo ya imani ili kuona yasiyoonekana.